Wanachama wavutiwa na teknolojia ya PSSSF kidigitali

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:59 PM Jul 01 2024
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charle Kichere (kushoto), akipokea kijitabu cha Mwongozo wa Mwanachama kutoka kwa Afisa Mkuu wa Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul Njaidi alipotembelea banda PSSSF.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charle Kichere (kushoto), akipokea kijitabu cha Mwongozo wa Mwanachama kutoka kwa Afisa Mkuu wa Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul Njaidi alipotembelea banda PSSSF.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umesema kumekuwa na muituikio mzuri wa Wanachama kutumia mtandao kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko.

Akizungumza kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Julius Nyerere maarufu Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam Julai 1, 2024.

Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF, Rehema Mkamba amesema “Kwa sasa tunasema PSSSF Kidijitali zaidi, tunawahamasisha wanachama wetu kutumia PSSSF Kiganjani Mobile App na PSSSF Member Portal ulipo Mtandaoni, ili kupata huduma zinazotolewa na Mfuko bila ya Mwanachama kufika kwenye ofisi za PSSSF.” amefafanua.

1
Miongoni mwa Wanachama wa PSSSF waliofika katika banda la PSSSF na kufurahiswa na huduma ya  PSSSF Kidijitali  ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Charles Kichere.

Akiongozwa na Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF, Abdul Njaidi na Afisa Huduma kwa Wateja Nahira Mang’ana, Kichere alioyeshwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF Kidijitali, ambapo kupitia simu yake aliweza kuskani QRCORD ya PSSSF Kiganjani Mobile App.