WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amezindua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kainam iliyoko mkoani Manyara yenye kidato cha tano na sita ambao una thamani ya zaidi ya Sh. millioni 400.
Akizungumza leo mkoani humo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi Waziri Kitila amesema lengo la mradi huo ni kuongeza miundombinu ya kidato cha tano na sita na kutoa nafasi kubwa ya wanafunzi wengi kupata fursa ya kujiunga na masomo kwa ngazi hiyo.
Mkuu wa shule hiyo Emanuel Nikodemus wakati akieleza maendeleo ya mradi huo amesema shule hiyo ilipokea kiasi cha Sh. millioni 428,9000 mwezi Mei, 2023 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili, madarasa sita na matundu tisa ya vyoo ambapo matundu yaliyojengwa ni 10.
"Mradi huo umeleta manufaa kwa wanafunzi na wadau wa elimu shuleni hapa na imesaidia kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutoka wanafunzi 44 hadi kufikia wanafunzi 612," amesema.
Waziri Kitila yuko mkoani Manyara kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa huo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED