Benki ya Akiba yatoa elimu ya fedha kwa wadau mbalimbali

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:10 PM Jun 17 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,  Silvest Arumasi.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Silvest Arumasi.

Benki ya Akiba imesema itaendelea kuunga mkono serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea kukua kwa uchumi wa Taifa.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki Jijini  Dodoma  na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,  Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali  lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na kujibu maswali na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji.

Upendo Makula, Meneja wa Tawi la ACB - Dodoma.
Mkurugenzi Arumasi alibainisha kuwa benki hiyo itawaangalia wananchi wa Dodoma kwa upekee kutokana na fursa mpya zilizopo katika Jiji hilo kwani serikali  imekuwa ikiendeleza na kustawisha Makao makuu ya nchi hivyo ametoa rai kwa wananchi  kujishughulisha na biashara na wanapokwama benki hiyo ipo kutoa  mikopo kwa riba nafuu .

"Tunaahidi kuwa benki itaendelea kuunga mkono serikali kwa kuwasadia wananchi kuwapatia mikopo nafuuu  ili kuinua mitaji yao pia kupanua wigo wa huduma nchi nzima ili kufikia azma ya kutoa mchango mkubwa  wa kuwepo kwa huduma shirikishi za kifedha yaani financial inclusion" alisema

Washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali.

Naye  Upendo Makula,  Meneja wa Tawi la ACB - Dodoma  aliwashukuru washiriki wote kwa kuitikia mwito  kwa ujumla wao.

Aidha washiriki wote waliishukuru benki hiyo kwa mada nzuri za semina hiyo na wameahidi kutumia elimu hiyo kama chachu katika utendaji wao wa kila siku kwani wamejengewa    msingi imara  wa uelewa wa maswala ya fedha

Washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali.