MAGOLI matatu yaliyofungwa na Clement Mzize, kiungo mshambuliaji Mudathiri Yahya na mshambuliaji Kenedy Musonda waliyoyafunga dhidi ya Mtibwa Sugar yametosha kuipa Klabu ya Yanga ubingwa wa tatu mfululizo Ligi Kuu Bara na kuwa mabingwa kwa mara 30.
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Mei 13, 2024 katika Uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mkoani Mogogoro.
Mchezo huo uliokuwa wa muhimu pia kwa Mtibwa wa kujinasua kushuka daraja na Yanga kutaka kutangazwa kuwa mabingwa msimu wa tatu mfululizo.
Matokeo hayo yamekuwa kitanzi zaidi kwa Mtibwa Sugar ambapo katika michezo 27 wamekusanya pointi 20 na kuendelea kusalia mkiani mwa ligi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED