Bondia Changalawe aingia kambini kujifua

By Shufaa Lyimo , Nipashe
Published at 01:05 PM Apr 28 2024
BONDIA wa mchezo wa ngumi za ridhaa, Yusuph Changalawe.
PICHA: MAKTABA
BONDIA wa mchezo wa ngumi za ridhaa, Yusuph Changalawe.

BONDIA wa mchezo wa ngumi za ridhaa, Yusuph Changalawe amesema wiki ijayo anatarajia kuanza kambi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kuwania kufuzu michuano ya Olympiki yatakayofanyika nchini Thailand kuanzia Mei 20 mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe, Changalawe amesema lengo lake ni kufanya vema kwenye mashindano hayo ili apate nafasi ya kwenda nchini Ufaransa kushiriki Olympiki itakayoanza Julai mwaka huu.

"Malengo yangu ni kupata nafasi ya kwenda kushiriki Olympiki nchini Ufaransa na kuweza kuipeperusha vema bendera ya Taifa,” amesema Changalawe.

Bondia huyo Ameongeza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kuwa na mataifa mbalimbali.

"Mashindano yatakuwa magumu, hivyo ninapaswa kujinoa kweli kweli ili nikatimize malengo iliyojiwekea,” amesema bondia huyo.