Waziri Ndumbaro atangaza fursa lukuki tamasha la tatu la utamaduni Ruvuma

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:43 PM Sep 17 2024
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ameeleza kuwa, Tamasha la tatu la Utamaduni la Kitaifa Songea litatoa fursa lukuki kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma na mikoa ya jirani katika nyanja za kibiashara, bidhaa za asili, vyakula, malazi, usafiri na litaambatana na mafunzo, semina na midahalo mbalimbali kuhusu Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.