MWAKA unapomalizika tahadhari za kiafya ni muhimu kuzizingatia na kufahamu cha kufanya ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali mojawapo ni tatizo la sasa la afya ya akili.
Wapo wengi wenye changamoto hiyo na mwanzo wa mambo hayo ni matokeo ya athari mbaya kwenye ubongo. Kumbuka kulinda ubongo na kuutunza.
BBC inajadili tabia 11 zinazoharibu ubongo wako na jinsi ya kuzishinda.
Ni taarifa zinazokusanywa kutoka kwenye ripoti mbalimbali za utafiti, zikiwamo za Shule ya Kitabibu ya Harvard na Taasisi ya Kitaifa ya Marekani ya Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu na Kiharusi (Neurological and Stroke).
Kuna mengi ya kuzingatia na ya kuepuka kuanzia ulaji na utendaji mzima wa maisha ya kila siku mojawapo ni:
KUKOSA USINGIZI
Usingizi usio wa kutosha, unatajwa na Kituo cha Sayansi ya Mfumo wa Mishipa ya Fahamu cha Marekani kuwa uharibifu mkubwa zaidi kwa ubongo unasababishwa na kukosa usingizi wa kutosha.
Usingizi wa kutosha kwa watu wazima unamaanisha saa saba hadi nane za usingizi kati ya saa 24 kwa siku. Wataalamu wanasema kuwa kulala mfululizo usiku ni bora zaidi.
Ubongo hupumzika baada ya kulala. Pia, huunda seli mpya wakati huo. Lakini ikiwa unalala chini ya saa saba, seli mpya haziundwi.
Hatimaye, haukumbuki chochote. Unapata ugumu wa kuzingatia, wa kufanya maamuzi. Kukosa usingizi huongeza shida ya akili.
Ikiwa unataka kulinda ubongo wako, kuna suluhisho moja. Pata angalau saa saba za kulala kila usiku. Japo saa nane za kulala ni bora zaidi.
Ili kufanya hivyo, unahitaji kwenda kulala angalau saa moja kabla ya kusingiza. Usitumie kifaa chochote wakati huo.
Safisha chumba cha kulala kabla ili kuunda mazingira ya usingizi. Punguza mwanga ndani ya chumba weka kila kitu vizuri.
Usilale na kufunika uso ni kwa sababu utazuia mwili kupokea oksijeni na kutoa kaboni kupitia pua.
Ukijifunika unaweza kusababisha kaboni kujilimbikiza karibu na uso matokeo yake ni uwezekano wa ukosefu wa oksijeni ukiwa usingizini.
KIFUNGUA KINYWA
Kumbuka hujala usiku kucha, kifungua kinywa lazima uanze nacho. Kunywa chai na vitafunio kwa sababu hutoa nishati ya kufanya kazi siku nzima.
Kuacha kifungua kinywa kunapunguza viwango vya sukari kwenye damu, jambo ambalo huathiri ubongo.
Kutopata kifungua kinywa siku baada ya siku husababisha uharibifu wa ubongo, hupunguza ufanisi wa seli.
Ukosefu wa virutubisho hufanya iwe vigumu kwa ubongo kufanya kazi kwa kawaida.
KUTOKUNYWA MAJI
Asilimia 75 ya ubongo ni maji ili kuweka ubongo katika hali ya unyevu maji ni muhimu sana kwa utendaji kazi wake bora.
Ukosefu wa maji husababisha tishu za ubongo kupungua na seli kushindwa kazi, hali hiyo
inaweza kupunguza uwezo wa kufikiri kimantiki au kufanya maamuzi.
Kwa mujibu wa wataalamu, mtu mzima anapaswa kunywa angalau lita mbili za maji kila siku kudumisha afya ya ubongo.
Unywaji maji unaweza kuongezeka kulingana na uzito, afya, umri, mtindo wa maisha na hali ya hewa.
KUENDEKEZA MSONGO
Kuwa na msongo wa mawazo wa hali ya juu na wa muda mrefu husababisha seli za ubongo kufa na sehemu ya mbele ya ubongo kusinyaa. Inaathiri kumbukumbu na uwezo wa watu kufikiria.
Kulingana na watafiti, watu ambao wamezama kila wakati katika kazi. Hawawezi kusema 'hapana' kwa wengine ikiwa watatakiwa wafanye jambo fulani. Watu kama hao wanakabiliwa na mafadhaiko zaidi.
Lakini acha kufanya hivyo, epuka kuchukua mzigo wa ziada kwa njia yoyote.
Hata wanapokuwa wagonjwa, watu wengine huendelea kufanya kazi za kuushughulisha ubongo, vinginevyo, utafiti umebaini kuwa ina athari mbaya za muda mrefu kwenye ubongo.
Kukaa katika sehemu moja kwa muda mrefu kunaweza kusababisha msongo zaidi.
Mbali na hayo, kukaa nyumbani hata siku za likizo ni jambo jema.
Kutofanya harakati za kutosha au kazi za mikono, inaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na kisukari na tatizo la afya ya akil.
Kwa hiyo ili kuweka ubongo wenye afya, fanya mazoezi ya kawaida, uinuke kutoka kwenye kiti chako kila nusu saa, unaweza kuweka saa ya kengele kwa ajili ya hiyo, kimbia au tembea kwa nusu saa angalau siku tatu kwa wiki.
ULEVI TEKNOLOJIA
Kama unavyoweza kukumbuka, kizazi kilichotangulia mara nyingi kilifanya hesabu ndogo bila kutumia vikokotoo. Kilikuwa kinakumbuka namba nyingi za simu, majina ya watu, visa mikasa na hadithi tele. Leo ni tofauti.
Tabia hizi ni kama mazoezi ya ubongo, ambayo huweka nguvu zake za kufikiri na kumbukumbu imara kwa muda mrefu.
Lakini katika zama hizi huhitaji kukumbuka sana, unatumia zaidi teknolojia na hasa ‘Google’ hilo limepunguza uwezo wa ubongo kufanyika.
Kumbukumbu na uwezo wa kufikiri unazidi kuwa dhaifu siku baada ya siku.
Ungependa kuuweka ubongo wako katika hali ya kuchangamka, kumbuka mambo bila kutumia Google, watafiti wanapendekeza.
Unatakiwa kucheza michezo tofauti kushughulisha ubongo. Kama mafumbo.
BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED