WIKI iliyopita ilikuwa na sehemu ya simulizi Tanganyika mpya ilikotoka hadi kufika mwaka 1964, ikianza na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitatu, iliyotimu mwaka 1964.
Mahudhurio yake alilenga sura kuu mbili, upande mmoja kubomoa misingi ya utawala wa kikoloni iliyokuwa na vikwazo katika matumizi ya rasilimali nchini mwao, mathalani fursa za kielimu.
Pia, ndani ya mpango huo, kukawekwa msingi ya mahitaji ya lazima yaliyoamuliwa kwa haraka, hasa katika matumizi ya mahitaji ya msingi kama vile afya, elimu, kilimo na matumizi ya ardhi.
Kutoka tafsiri pana, Tanganyika haikuwa koloni la kudumu na kwa maana hiyo, Wajerumani waliopokelewa baadaye na Waingereza hadi Uhuru, hawakuwekeza kwa kina, wakijua walikuwapo kipindi cha mpito.
Hiyo iliwafanya wawekeze katika mahitaji ya lazima, yaliyowawezesha kunufaika na nchi, ikiwamo uzalishaji malighafi mengi, yakiwamo kahawa na katani.
Mpaka Tanganyika inapata uhuru, kulikuwapo viwanda vichache na elimu shuleni inatolewa kwa ubaguzi, nafasi kubwa wakipata watoto wa Kizungu, kufuatiwa na Kiasia na Waafrika walipata nafasi kidogo, wengi wakibaki nyumbani.
Yote yalifanywa hadi Uhuru na miaka mitatu baadaye, nchi ikijipanga kujikwamua kutoka madhila ya ukoloni, sura kuu ya uchumi yaliyokuwa magumu kukosa huduma, sura ya uzalishaji kitaifa ikiwa “tunazalisha tusichokitumia na kutumia tusichozalisha.”
MAZITO YA 1964
Ilipotimu mwaka 1964, Tanganyika ilifanya mageuzi makubwa ambayo mantiki na msingi yake hadi sasa, inabaki kuwa mithili ya katiba kuu kitaifa, jumla yako manne.
Mosi, ni kuundwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayotokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa lugha rahisi, ikaundwa taifa imara zaidi kusalama, kijamii, siasa na uchumi, huku muundo wake ukibaki ni muungano wa kipekee kimataifa.
Pia, kuna kinachoenda karibu nayo ni kuundwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo lina historia kubwa katika kulinda nchi na ukombozi wa Afrika, ikibeba sifa hadi sasa weledi na uadilifu.
Eneo la tatu, penye sura kuu ya uchumi na maendeleo, ni pale Tanzania Bara ilipounda Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 1964 hadi 1965.
Hali kadhalika, uamuzi wa mwisho uligusa kuingiwa mfumo wa chama kimoja cha siasa, ikitafsiri aina ya kisiasa ya nchi, inayoangukia mlengo wa kushoto, itikadi ya kijamii, kitaifa kukitumika falfasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Maudhui ya kiuchumi ya mpango huo miaka mitano, pia yaliegemea kusudio la kijamaa, mali na uchumi mkuu wa nchi kumilikiwa na serikali.
MPANGO 1964-69
Huo ndio ukawa msingi wa kidumu namna nchi iliendeshwa na miaka yote 50 hadi sasa, Tanzania yote inatumia muundo huo. Kwa kifupi, imebaki kama katiba ya kiuchumi na kisiasa kwa muungano wote.
Hata inapoingiwa kwa kina, urafiki wa viongozi wakuu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume, ulioanza hata kabla ya uhuru, mbinu na maudhui hayo ya ‘bidhaa’za mpango huo, yalionekana Zanzibar kwa manufaa ya Wazanzibari.
Wakati huo, maendeleo ya nchi yakiwa changa na mambo mengi yako nyuma, Mpango wa Maendeleo 1964- 1969, ulilenga kuinua mambo ya msingi kwa Watanzania walioko katika maisha ya msingi.
Ni zama ambazo wastani wa asilimia 90 ya Watanzania walikuwa wakulima vijijini, maeneo ambako yalikuwa na huduma duni, ikiwamo miundombinu ya msingi kama vile barabara.
Wengi hawakupata kabisa fursa za elimu ya msingi, hali kama hiyo katika huduma za afya na ardhi. Huku mifumo yao ya kilimo na ufugaji, eneo ambalo limedumu hadi sasa kuwa nguzo ya uchumi wa nchini, baadhi yakiwa na majirani wa utalii nguzo nyingine ya uchumi na fedha za kigeni.
Katika utekelezaji wa mpango huo wa kwanza, Rais Nyerere, kwa kutumia mikakati ya ndani na nje, akaanzisha uwekezaji mkubwa kupitia mpango huo ulioazimia kuwapo muundo maaluma wa vijiji, nia ni kuunda huduma kama zahanati na shule za msingi, ambako ndio kulikuwa angalizo lake kuu.
Mtaji wa uwekezaji wake Rais Nyerere, alichukua sura kuu tatu. Kwanza kutumia mapato ndani ya nchi, kutafuta msaada wa kigeni, hasa nchi rafiki za kijamaa kama iliyokuwa Jamhuri ya Muugano wa Kisovieti (USSR) na China, ambayo ni marafiki kimaendeleo nchini hadi sasa.
Vilevile, tafsiri ya uendeshaji ‘ujamaa halisi’ ulitekelezwa mwaka 1967, ikatengenezea nchi mtaji zaidi mtaji wa maendeleo kupitia utaifishaji wa mali binafsi.
Ikipewa tafsiri kutoka tamko la chama – TANU kwamba “ni njia sahihi ya kuendesha taifa sawa na huru” kukishuhudiwa mali nyingi za umma kuzalishwa, ikiwamo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) iliyotokana na fedha ya kigeni.
Aidha, shirika la umma lililoitwa Msajili wa Majumba, majengo yake mengi yakiwa maghorofa mijini, makazi na ofisi yatokanayo na utaifishwaji wa Azimio la Arusha, yakaunda ajira na makazi mpya.
Ni zama ambazo misaada ilimiminika nchini na viwanda vingi kujengwa za kuzalisha mahitaji ya nchini, kufuta ‘tunazalisha tusichoagiza na kuagiza tusichozalisha,’ mathalan Dar es Salaam, ndio ukawa mzizi wa kumea viwanda katika Barabara ya Pugu (sasa Barabara Nyerere).
Vilevile, pengo kubwa la upatikanaji wa nguo nchini, kuwanusuru Watanzania na shida ya nguo, ghafla kunamea mipango na ushuhuda wa kujenga viwanda vya nguo kama Urafiki, ambao siri ya ujenzi wake mwishoni mwa miaka ya 1960, mtaji ulitokana na urafiki kati ya Tanzania na China.
Mengine ni majina kama; Tabotex (Tabora), Mutex (Musoma), na Kiltex ya Dar es Salaam, iliyoendana na kueneza umaarufu, utamaduni na siasa wa nchi katika vazi la khanga ukidhihirisha dhana ya wiki wiki iliyopita katika makala hii “Siasa na Uchumi na Uchumi ni Siasa.”
Ndani ya mikakati hiyo na mipango tajwa ya kupanua viwanda, ikaunda nafasi mkutanua fursa za ajira nchini, ukitumika mfumo uliojulikana “Labour Intensive System,” kwamba namna ya uzalishaji viwandani, mashine zinatumia nguvu kazi zaidi, tofauti na inayoitwa ‘Capital Intensive,” ikizama katika mashine.
Matokeo yake, ndani ya miaka hiyo mitano, kukaibuka kundi kubwa la wafanyakazi viwandani, huku serikali ikiajiri kwa kasi watumishi wa umma na wakati huo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), watumishi wake walianza kuingia mtaani.
Kimsingi, katika miaka mitano kabla ya uhuru, kulikuwapo waajiriwa wachache sana wasomi katika utumishi wa serikali, huku walio na shahada za juu wanahesabiwa.
Katika kukabili hayo kwa haraka, ndani ya mlango huo wa kwanza, Rais Nyerere, akachukua juhudi kuanzisha vyuo vya utendaji kibiashara na kiutawala na ndio ikawa chanzo cha kuundwa kama Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam.
Nako katika uzalishaji malighafi nma ajira vijijini, serikali iliongeza juhudi katika sekta ya kilimo ambako vyuo vilivyokuittwatangu uhuri na baada yah apo, ambavyo sasa vinaunda vyombo viitwavyo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI).
Hapo wakapatikana mabwana shamba na mabibi shamba waliosambazwa shambani, kuinua kilimo chao kila mahali na kasi ya uzalishaji chakula na malighafi kuongezeka zaidi na upande wa vijana, kubunjwa taasisis za kuhudumia umma zikawa nyingi sana.
Wakati mpango huo wa miaka mitano unafika tamati mwaka 1969, kukawapo mashirika mengi ya umma nchini, kundi kubwa nkla wafanyakazi, kilimo kimepamba moto nchini sasa taifa kilichukua sura ‘kukitumia tunachokizalisha.”
Serikali ikaamua kuunda sheria inayosimamia wafanyakazi na mashirika ya umma na ndani yake kukaundwa Tume ya Rais ya Kusimamia Mashirika la Umma inayoitwa (SCOPO).
Ndani ya sheria inayosimamiwa na SCOPO ilikuwa na mengi yanayomhusu mfanyakazi, maslahi na cheo chake, hata ikiupa umaarufu msamiati ‘Mshahara wa SCOPO.”
· Inaendelea Ijumaa ijayo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED