Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama cha ACT- Wazalendo, Abdul Nondo, amedai baada ya kuachiwa na watekaji, walimtishia asiseme lolote la akifanya hivyo, watamuua.
Nondo anayedaiwa kutekwa Desemba mosi mwaka huu Stendi ya Mabasi ya Magufuli baada ya kuteremka kwenye basi akitokea mkoani Kigoma, amedai kwamba alichukuliwa kwa nguvu na watu sita ambao walimfunga mikono na miguu pamoja na uso na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Watekaji walinichukua kwa nguvu, licha ya kelele na vuta nikuvute. sikusaidika na kulikuwa na bodaboda moja na watu wengine wakiangalia tukio lile likiendelea lakini hawakunisaidia.”
“Walinifunga kitambaa cheusi kwenye macho, kamba mikononi… walinisafirisha kwa mwendo huku nikipigwa na baadaye walinining`iniza mahali, miguu juu huku wakinipiga kwenye unyao wa miguu, walinipiga mgongo na mikononi.
“Nilitolewa na kubadilishwa kwenye gari nyingine… wakanifungua pingu, wakanifunga kamba na kunining`iniza kwenye gari ndogo kutoka ‘hardtop’ kisha kunisukumiza kwenye fukwe hizo wakaondoka…nilihisi upepo na mawimbi ya bahari, ndipo nikapata msaada kwenda katika ofisi za chama,”amesema Ndondo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED