KLABU ya Rotary Masaki kwa kushirikiana na Rotaract E-Club ya Dar es Salaam na Rotaract Club ya TIA, wameratibu kambi ya matibabu ya macho kwa wanafunzi na wazazi wa Shule ya Msingi Bunge.
Rais wa Rotary E-Club ya Masaki, Kaushik Bhojak , akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kambi hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Novemba 30, 2024, amesema lengo ni kutoa huduma muhimu za afya ya macho kwa watoto na jamii hiyo.
“Kwa kuishirikiana na wadhamini wetu benki ya DTB, Travelport na Lalji Foundation tumefanikiwa kutoa huduma ya matibabu kwa watu 360 katika kambi yetu tuliyofanya leo katika Shule ya Msingi Bunge,” amesema.
Amesema pia wametoa dawa kwaajili ya wagonjwa waliokutwa na matatizo mbalimbali na kupatiwa huduma nyingine kama vinywaji na vichangamsha kichwa vingine.
“Kambi hii ya matibabu umetolewa kwa moyo wa upendo na Yusuf Medics (Shamshu Pharma), ili kuhakikisha watoto wanaokuwa na mahitaji maalum wanapokea matibabu yanayofaa
“Tukio hili limeacha alama isiyofutika, ikiwa ni mfano bora wa umuhimu wa huduma za afya za kijamii,” amesema Bhojak.
Kambi hiyo ilikuwa ishara ya mshikamano na kujitolea, ikiangazia jinsi ushirikiano wa mashirika mbalimbali unavyoweza kuboresha maisha ya watoto na jamii kwa ujumla.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED