Wakulima wa Mkonge wakaribishwa kujifunza kilimo cha faida 77

By Mary Geofrey , Nipashe
Published at 12:15 PM Jul 08 2024
Raia wa China, akikagua nyuzi za zao la Mkonge, alipotembelea Banda la Bodi ya Mkonge (TSB) katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam
PICHA: MPIGAMPICHA WETU
Raia wa China, akikagua nyuzi za zao la Mkonge, alipotembelea Banda la Bodi ya Mkonge (TSB) katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam

BODI ya Mkonge Tanzania imehamasisha wananchi kulima zao la Mkonge kwa wingi kwasababu soko lake ni kubwa na la uhakika.

Aidha, kiwango cha uzalishaji wa zao hilo bado ni kidogo kwasababu wakulima wengi hawazingatii kanuni za kilimo cha zao ho.

Ofisa Masoko, Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB)  David Maghali, ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika Maonesho 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Maghali amewakaribisha wakulima wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta hiyo kuingia mwenye zao hilo linalovunwa miaka mitatu baada ya kupandwa.

REA..jpeg 83.34 KB
"Mkonge una fursa nyingi ukiachana na kilimo unaweza kuwekeza kwenye mashine za uchakataji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo. Kwa yoyote anayetaka kuwekeza kwenye kilimo hiki tunamkaribisha kwenye banda letu hala sabasaba tuwekeze kumwelekeza aweze kunufaika na fursa zilizopo," amesema Maghali.

Kuhusu changamoto amesema wakulima wengi hawazingatii kanuni za kilimo ikiwamo kutumia eneo kubwa kwa kilimo na kupata mazao machache.

"Kilimo bora ni kuandaa shamba kwa kuondoa visiki na kupitisha trekta pamoja na kupalilia mara tatu hadi nne kwa mwaka ili majani au miti isizonge mmea," amesema.