WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema hakuna anayeweza kuongoza Tanzania zaidi ya Samia Suluhu Hassan.
Sumaye aliyasema hayo leo wilayani Hanang, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, anayetembelea mikoa mitano.
“Hakuna mtu mwingine anayeweza kuongoza hii nchi zaidi ya Samia Suluhu Hassan, acha nje ya CCM hata ndani ya CCM, hakuna mtu atakayeiongoza hii nchi, atayeiendesha kama inavyokwenda zaidi ya Samia Suluhu Hassan.
“Hata ndani ya CCM hayupo, sembuse nyie nje kuna nini! Husikii wenyewe wameparura hovyo hawajapata madaraka wanaparurana,wakipata si tutakoma, amesema Sumaye.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED