Serikali inaendelea kuchunguza chanzo cha moto kilichotolea kata ya Ngarenairobi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro na kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu.
Hayo yamesemwa leo na Mbunge wa Jimbo la Siha (CCM) ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, wakati wa mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Roseline kata ya Ndumeti wilayani Siha.
Dk. Mollel alipofika kata ya Ngarenairobi aliwafariji wahanga hao huku akiwahakikishia watoto wao kuendelea na masomo na huduma muhimu kwa wananchi watapatiwa.
Amesema wananchi ambao wamepata ajili ya kuunguliwa nyumba zao wametakiwa kuwa watulivu kwa kuwa serikali inaendelea kuchunguza tukio hilo ili waendelee na maisha yao ya utafutaji.
Tukio hilo lilitokea Julai 6 mwaka huu nyumba yenye vyumba 11 vya wapangaji viliteketea kwa moto na kusababisha hasara.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED