MATUMIZI ya Mtandao wa WhatsApp ni miongoni mwa ulio kinara katika utangazaji kwenye mitandao ya kijamii, ukiwa na watumiaji milioni 9.9.
Utangazaji kwenye mitandao ya kijamii nchini unafikia asilimia 33, ukitanguliwa na mtandao wa WhatsApp, Facebook (mil 8.1), Instagram (mil 3.7), YouTube (mil 2.9), Tik Tok (1.6) kisha X (zaidi ya laki saba).
Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka, ameyasema hayo leo, Dar es Salaam akiwasilisha mada kuhusu Wajibu na Majukumu ya Vyombo vya Habari Kuelimisha Umma.
Mkutano huo wa siku mbili, umeandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji daftari la kudumu la wapigakura awamu ya kwanza, ukiwakutanisha waandishi wa habari takribani 200 wa mkoa huo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED