KATIBU wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla,amewaomba radhi wanachi wa Longido kwa kauli ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marco Ng'umbi kwamba zililenga kuwachonganisha.
Akizungumza na wananchi katika eneo la Kilimahewa Kata ya Mundarara, amesema chama hicho kinaheshimu uchaguzi wa haki na kushinda kwenye sanduku la kura na sio vinginevyo.
"Hayo (kauli za DC) yameshapita,zile zilikuwa kauli zake yeye,sijui alienda porini kufanya nini kama alienda kutafuta shamba au kuchimba dawa anajua yeye,"amesema.
Amesema CCM inajivunia utekelezaji wa Ilani ya CCM,hatuhitaji mbeleko,hapa ni ngome yetu hivyo hakukua na sababu za kutofuata misingi ya uchaguzi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED