KATIBU wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Longido Samia,kusoma kwa bidii na kuwa waadilifu ili wawe viongozi wa Tanzania baadaye.
Akizungumza leo Septemba 5,2024 na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Longido Samia Girls, Kata ya Rubomba,Wilaya ya Longido,mkoani Arusha alisema bidii na nidhamu ndio msingi wa mafanikio kwenye maisha ya masomo na kazi.
"Tupo hapa kuona ujenzi wa shule hii,napongeza sana kazi nzuri iliyofanyika hadi majengo haya yamekuwa hivi.Tunqmshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kwa vitendo namna analeta mageuzi katika sekta ya elimu,"amesema.
Amesema zamani 'High school' zilikuwa chache lakini Arusha waliamua ijengwe Longid,ni furaha kubwa tunamshukuri Rais,mbunge.Majengo mazuri,ili elimu iwe nzuri kunahitajika majengo,waliku na wanafunzi.
"Kutokana na uwepo wa shule hiyo ni nafasi ya kuthibitisha ndoto na dhamira zao (wanafunzi) wanataka wawe nani ktika nchi hii,wazingatie kilicjowalewa,serikali itatimiza wajibu wa mazingira mazuri ya kusoma,wakae mahali salama na kupata walimu.jukumu la kubadilisha maisha yako (mwanafunzi) unaipata shuleni,"amesema.
Zingatieni hilo nyie ni wataalam mnaokuja,nimeelezwa Rais kaleta mil 350 kukamilishaa ujenzi wa Bwalo ambalo ndio changamoto kubwa,na nyingine ni uzio.
"Hili ni jambo nyeti tutalifanya kwa Halmashauri kupitia mapato ya ndani kutafuta vyanzo,pia tutaongea na Waziri wa TAMISEMI kutenga fedha,tuwaombe wadau watuchangie ili tujenge uzio kwa ajili ya usalama wa watoto.Usalama ni muhimu sana,naamini Mkuu wa wilaya atalisimamia hilo,"amesema.
Aidha,amesema ameelezwa kuhusu changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara na kuwaomba wadau kujitokeza kuleta umeme wa jua kama mbadala wa kupata nishati kwa ajili ya wanafunzi.
"Natoa nafasi kwa mdau yeyote popote alipo ajitokeze,nipo tayari kuja kupokea msaada huo,akitokeze aweke umeme wa jua hapa ili kuondoa changamoto ya umeme,"amesema.
Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha,Adelhem Mkulu, amethibitisha uwepo wa tatizo la umeme ambalo linashughulikiwa kwa kukamilika kwa kilometers 1,000 wameanza ujenzi wa kutuo kipya cha kupooza umeme,na kwamba Longido italishwa umeme kutokea Karatu ili kumaliza tatizo lililopo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED