Binti wa Jacob Zuma achumbiwa na Mfalme Mswati III

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 05:27 PM Sep 03 2024
Nomcebo Zuma (21), akiwa na baba yake Jacob Zuma (82).
Picha:Mtandao
Nomcebo Zuma (21), akiwa na baba yake Jacob Zuma (82).

BINTI wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni miongoni mwa mamia ya wanawake na wasichana waliocheza ngoma kwa ajili ya Mfalme wa Eswatini katika sherehe za kitamaduni juzi, kuthibitisha uchumba wake na mfalme huyo.

Binti huyo ambaye ni Nomcebo Zuma (21), alikuwa miongoni mwa watu 5,000 kutoka katika ufalme huo mdogo katika sherehe maarufu kama 'Reed dance' ya kila mwaka katika Kijiji cha Kifalme cha Ludzidzini huko Lobamba, kusini mashariki mwa mji mkuu Mbabane.

Ilielezwa kuwa japokuwa sherehe hiyo ya siku nzima ni ya kitamaduni kwa mwanamke, imefanyika wakati ambako Mfalme Mswati (56), anaweka wazi chaguo lake la mke mpya.

Tayari ana takriban wake 14, baadhi yao aliwaoa walipokuwa wadogo, na ana takriban watoto 25.

Aidha, wiki iliyopita, kaka yake Mswati alisema kuwa Nomcebo Zuma atahudhuria Ngoma ya Reed kama "Ngoma ya Reed  ambayo ina maana ya mchumba wa kifalme.

Katika hafla ya jioni ya Jumatatu, alikuwa miongoni mwa mamia ya wasichana waliovalia mavazi ya kitamaduni, wengine wakiwa na mapanga na ngao za kuigwa, ambao walicheza mbele ya Mswati na msafara wa wanaume waliovalia ngozi za kitamaduni.

Baba yake Jacob Zuma (82), pia ana wake wengi kutokana na mila zao na watoto takriban 20. Alilazimika kujiuzulu kama rais wa Afrika Kusini 2018 chini ya wingu la tuhuma za ufisadi.

Chanzo: Mtandao