Wataka sheria za biashara ziainishwe peke yake dira 2050

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 02:37 PM Jan 08 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za GSM, Benson Mahenya.
Picha: Mauld Mmbaga
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za GSM, Benson Mahenya.

WAFANYABIASHARA na wamiliki wa kampuni nchini wamependekeza sheria zinazohusiana na biashara kuainishwa peke yake kwenye rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kuepuka changamoto zinazojitokeza kutokana na sheria hizo kuingiliana na nyingine.

Hayo yamesisitizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za GSM, Benson Mahenya kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara na Wamiliki wa kampuni kuhakiki rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, leo Jijini Dar es Salaam.

Amesema suala hilo linasababisha baadhi ya biashara kutokwenda ipasavyo, na kwamba kuna haja ya kufundisha elimu ya biashara kuanzia chekechea hadi vyuoni ili kuhakikisha vijana wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala ya biashara.

Katika hatua nyingine, amesikitishwa na serikali kuweka mkazo zaidi kwa watoto wa kike ukilinganisha na watoto wa kiume jambo ambalo amedai kuwa ni hatari kwa maendeleo ya Taifa, huku wakipendekeza Dira 2050 kuliangalia suala hilo ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza mbeleni.

1