Wahasibu wakuu wa serikali Afrika kukutana Arusha

By Cynthia Mwilolezi , Nipashe
Published at 08:20 PM Jul 24 2024
MHASIBU Mkuu wa Serikali nchini CPA Leonard Mkude akizungumzia mkutano mkuu wa pili wa wahasibu wa serikali kutoka barani Afrika utakaofanyika Desemba 2 hadi 3 mwaka huu jijini Arusha.
Picha:
MHASIBU Mkuu wa Serikali nchini CPA Leonard Mkude akizungumzia mkutano mkuu wa pili wa wahasibu wa serikali kutoka barani Afrika utakaofanyika Desemba 2 hadi 3 mwaka huu jijini Arusha.

WAHASIBU Wakuu wa serikali Barani Afrika (AAAG) kutoka nchi 55 za Umoja wa Wahasibu Wakuu Afrika, wanatarajia kukutana Jijini Arusha katika mkutano mkuu wa pili utakaofanyika Desemba 2 hadi 5 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Arusha Mhasibu Mkuu wa Serikali Tanzania CPA.Leonard Mkude amesema lengo la mkutano huo ni kujenga imani ya umma katika mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwa ukuaji endelevu.

"Tunatarajia washiriki watakuwa zaidi ya 2000 ambao ni wahasibu,wakaguzi wa hesabu,wataalamu wa masuala ya fedha,Tehama,Vihatarishi na kada nyingine, wakiwemo walioajiriwa serijlaini,kampuni binafsi pamoja na walioko katika ajira binafsi,"amesema.

Amesema wageni wa nje pia watapata fursa kutembelea hifadhi mbalimbali nchini na vituo vya utalii ili wakasaidie kuwa mabalozi wa utalii kwenye nchi zao.

Aidha amesema baadhi ya faida za mkutano huo ni kuwa na Afrika yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji jumuishi na maendeleo endelevu.

Faida zingine ni Afrika yenye utawala bora,demokrasia,kuheshimu haki za binadamu nanutawala wa sheria  pamoja na Afrika yenye amani na usalama.

Mhasibu Mkuu wa Serikali Tanzania CPA.Leonard Mkude na (kushoto) Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika Malehlohonolo Mahase wakizungumzia juu ya mkutano mkuu wa pili wa wahasibu wakuu wa serijlai Barani Afrika urakaofanyika Desemba 2 hadi 5 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika, Malehlohonolo Mahase amesema  wameuleta mkutano huo mkuu kwa sababu Tanzania  ya kwanza katika utekelezaji wa  matumizi ya mifumo jumuishi ya usimamizi wa fedha na taarifa, ambazo  nchi za Afrika wanazotumia.

"Tuligundua kuwa Tanzania ni Taifa moja la mfano, kwa sababu imepiga hatua katika utekelezaji wa mfumo huo na  mfano katika utekelezaji wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma,"amesema.

Kadhalika, Tanzania imejaliwa kuwa na  vivutio vikubwa vya watalii, hivyo ni fursa kwa wanachama wao kwenda kutalii kwenye hifadhi mbalimbali za utalii na kufurahia vivutio hivyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha mikutano Arusha (AICC) Christina Mwakatobe, amesema ujio wa mkutano huo mkuu wa wahasibu Afrika ni fursa nzuri kiuchumi na uwekezaji.

WAANDISHI wa Habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika ukumbi wa Kituo cha mikutano ya kimataifa AICC jijini Arusha wakisikiliza ujio wa wahasibu wakuu wa serikali barani Afrika Disemba 2 hadi 5 mwaka huu.