Msongamano wa malori Saza Road Chang’ombe waanza upya

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:53 PM Jan 10 2025
Msongamano wa malori Saza Road Chang’obe waanza upya.
Picha:Mpigapicha Wetu
Msongamano wa malori Saza Road Chang’obe waanza upya.

WATUMIAJI wa barabara za viwandani hasa Mtaa wa Saza Changombe jijini Dar es Salaam wameelezea kurejea kwa kero ya msongamano wa malori kuegeshwa barabarani.

Wamesema malori hayo yamekuwa yakiegeshwa pande zote za barabara hali inayosababisha watumiaji wengine wa barabara kushindwa kupita na kusubiri muda mrefu.

Mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo, Anna Mlari amewataka askari wa kikosi cha usalama barabarani nchini kufika  eneo hilo kuona hali halisi, akieleza kuwa kunaweza kuwa na hatari iwapo janga la moto litatokea.

“Njia ya Saza Road na Mwakalinga muda wote malori yameegeshwa barabarani, tunapita kwa shida sana, na tunajiuliza iwapo itatokea dharura ya moto magari ya zimamoto yatapita wapi, TARURA, Polisi Temeke waje waone na kutatua kero hii,” amesema. 

Mtumiaji mwingine wa barabara hiyo, Mwita Kirai amesema wakati wa mchana na jioni hali inakuwa mbaya zaidi na hivyo amesisitiza wito wa kuchukuliwa hatua mara moja dhidi ya hali hiyo.