Wadau wahimiza ustawi jumuishi

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 02:40 PM Jan 10 2025
MKURUGENZI wa Taasisi ya Kiraia ya Civil Society Justice Novati.

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kiraia ya Civil Society Justice Novati amehimiza umuhimu wa kukuza uchumi shindani kuelekea miaka 25 ijayo ili kutoa hakikisho la nchi kuwa na ustawi jumuishi na ulio endelevu kwa vizazi na vizazi.

Justice amezungumza hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maoni yaka katika mkutano uliowakutanisha  asasi za kiraia kwa lengo la kuhakiki rasimu ya pili ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Pia Justice ameishukuru serikali kwa kuwajumuisha kwenye uandishi wa Dira 2050, akihimiza umuhimu wa ushindani kwa ngazi ya ndani ya nchi kuanzia ngazi ya mikoa kama ilivyo kwa mataifa jirani.

"Katika mataifa ya wenzetu Kaunti mbalimbali zimekuwa zikishindana kwa vigezo vya kutengeneza ajira mpya na ujumuishwaji wa makundi ya pembeni katika ustawi na ukuzaji wa uchumi, kama taifa si vibaya kuiga mazuri hayo," amesema.