EQUITY, Bakhresa group kukopesha wafanyabiashara kidigitali

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:34 PM Sep 26 2024
EQUITY, Bakhresa group kukopesha wafanyabiashara  kidigitali
Picha: Mpigapicha Wetu
EQUITY, Bakhresa group kukopesha wafanyabiashara kidigitali

BENKI ya Equity kwa kushirikiana na Kampuni ya Bakhresa group zimeingia makubaliano ya kukopesha wafanyabiashara ambao wanatumia bidhaa za kampuni hiyo.

Lengo ni kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga na  atakuwa na iwezo wakukopa fedha kwaajili ya kupata bidhaa hiyo hadi zaidi ya Sh. mlioni 300.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Equity, Leah Ayoub, amesema makubaliano hayo yalianza 2021.

“Tunajua wasambazaji na wajasiriamali wengi wanapata ya mitaji na kupata changamoto ya riba tukaona tunarahisishe huduma zetu kwa wateja na wasambazaji wa Azam.

"Mkopo huu hautakuwa na riba isipokuwa mteja atalipa kamisheni yakuanzia asilimia 0.5 mpaka 1.5 ambapo mkopaji atapaswa kulipa fedha hizo kuanzia siku saba hadi 30," amesema Leah.

Ameongeza kuwa, “Hii ni fursa ya kukuza mtaji wako kwa haraka,tumeamua kujitoa kwa wajasiriamali na kuwawezesha wapate huduma kwa urahisi bila vikwazo vingi ambapo mteja hata kama hana akaunti ya Equity ana uwezo wa kuifungua kiganjani mwake akapata mkopo.”

Naye Mkurugenzi wa Uhusiano wa kampuni Bakhresa Group, Hussein Sufiani, amesema makubalino haya yatamsaidia mteja ambapo badala kuhangaika kutafuta mfadhili au mdhamini wakumpatia fedha anaweza kwenda benki au kutumia mtandao kupata huduma.

“Hii nayo ni kidigitali,utapata huduma hiyo kwa mfumo wa sms (ujumbe mfupi),sio lazima uende benki kufanya transfer (kuhamisha) inafanyika moja kwa moja ukishafanya oda yako,kadri unavyozidi kukopa kiwango kinakua,”amesema Sufiani.

Amesema huduma hiyo itawasaidia zaidi wateja wao hasa wadogo hivyo amewahimiza kuchangamkia fursa hiyo.