Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dk. Joyce Nyoni, amepokea tuzo ya pili bora katika uandaaji wa taarifa za hesabu za kifedha kwa kundi la vyuo vya elimu ya juu.
Hafla ya utoaji tuzo hizo iliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) na kufanyika jana Novemba 29, 2024, katika Ukumbi wa APC Bunju, jijini Dar es Salaam.
Dk. Nyoni aliambatana na Mhasibu Mkuu wa Chuo, Aisha Kapande, pamoja na timu ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu za ndani wa Chuo cha Ustawi wa Jamii.
Tuzo hiyo ni ishara ya chuo hicho kuwa bora katika kuimarisha uwazi, ufanisi, na weledi wa uandaaji wa taarifa za kifedha.
Tuzo hizo za NBAA zinalenga kutambua taasisi zinazofanya vizuri katika usimamizi wa fedha na uwajibikaji, huku zikiwa chachu ya kuimarisha mifumo ya kifedha nchini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED