CCM yakoshwa mradi wa maabara ya kisasa ya kupima ubora wa maji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:01 AM Sep 26 2024
CCM yakoshwa mradi wa maabara ya kisasa ya kupima ubora wa maji

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wametembelea mradi wa Maabara ya kisasa ya kupima ubora wa maji ambao umetekelezwa na wataalamu wa ndani kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kamati hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka  Mhandisi Kija Limbe amesema kiasi cha Tshs;: 81,859,500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na ununuzi wa baadhi ya vifaa vya Maabara hiyo.

Mhandisi Limbe ameeleza pia mradi huu umetumia mapato ya ndani ya Mamlaka hiyo na mradi huo umekamilika kwa asilimia 100.

Aidha, Kamati hiyo imeweka wazi kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao thamani ya fedha zilizotumika zinaonekana.

1

Mradi huo unalenga kuhudumia zaidi ya wananchi 592,132 wanaohudumiwa na Mamlaka kwa eneo la Manispaa pamoja na Halmashauri ya Moshi.

Ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa  unalenga kuendelea kuwahakikishia wananchi usalama wa maji wanayokunywa kutoka bombani.