Mikakati yaundwa kuipandisha Timu ya Stand United Ligi Kuu

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 07:13 PM Jul 15 2024
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akitangaza kamati mbalimbali ambazo zimeundwa kwa ajili ya kuipandisha timu ya stand united kushriki kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara.
Picha: Marco Maduhu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akitangaza kamati mbalimbali ambazo zimeundwa kwa ajili ya kuipandisha timu ya stand united kushriki kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara.

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro ambaye ni mlezi wa timu ya stand united,ametangaza rasmi kamati mbalimbali ambazo zitatekeleza majukumu ya kuipandisha timu hiyo kushiriki kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara.

Kamati hizo zimetangazwa jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Michezo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.

Mtatiro kabla ya kuanza kutangaza kamati hizo ameishukuru Kampuni ya Jambo Food Product kwa kuipambania Timu hiyo ya Stand United kwa kuendelea kuifadhili hadi sasa ikiwa inacheza Ligi ya Championship.

"Leo tumekutana hapa kupeana mrejesho juu ya kikao kilichopita kwa kutangaza kamati mbalimbali ambazo zimeundwa ili kuendeleza timu yetu na kuipandisha kushiriki kucheza ligi kuu ya Tanzania bara," amesema Mtatiro.
 
Ametangaza kamati hizo kuwa Kamati ya fedha itakuwa na Mkuu wa Wilaya Julius Mtatiro, Seleman Hamis,Dk.Kalekwa Kasanga,Alexius Kagunze,Masudi Kibetu,Gasper Kileo,Patrobas Katambi, Ahmed Salum, na Lucy Mayenga,

Wengine ni Emmanuel Cherehani,Salome Makamba,Kija Makindo,Geogre Shujaa,Gilitu Makula,Ally Amour, Masalu Lusana na Khadija Kabojela.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (kulia)akimkabidhi Sh.milioni moja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro kwa ajili ya kuanza kuiunga timu ya Stand United.

Ametaja Kamati ya  Usajili na Mashindano, kwamba itakuwa na Musa Lyoba,Dk Hellyson Maeja,Sudi Juma,Juma Marwa,Jerry Julius,Chrispin Kakwaya,Stivian Antindius na Afande Tegemea.

Kamati ya Hamasa Itakuwa na Bihemo Thomas,Anord Rwekiza, Omary Malula,Madam Sitta,Issa Mbaraka,Zaituni Kiboga,na Sadi Bonge, huku kamati ya ulinzi ni Base Sunzu, Sadi Bonge,Sterwart Mathias,Fred Masai,Sospeter Kisobilo, na Peter Toshi.

Kamati ya Chakula Grace Joliga,Base Sunzu na Mbezi Kwilasa. na Kamati ya nidhamu na maadili ni Mzee Tendele,Wakili Kabudi,Mzee Gwama,Mzee Kazembe,na mtu mmoja kutoka Serikalini.

Kamati ya mapokezi ni Hamduni Khalfan,Michael Kaijage,Mseti Matiko,Sudi Juma,Mussa Lyoba,Chrispin Kakwaya na Stivian Antidius, na kamati ya ufundi ni Steward Mathias,Msafiri Patric na Ngassa Swaganya, ambapo kamati ya manunuzi ni Telezia Alois,Diana Msuya na mtu mmoja kutoka Serikalini.
1

Aidha,Mtatiro amewaomba wanachama wa Timu ya Stand United wajipange ili wawe na kadi za chama, na kwamba wana matarajio pia ya kufungua duka la kuuza bidhaa mbalimbali ambazo zitakuwa na nembo ya Stand United.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,amesema  kwa sasa timu ya stand united imepata viongozi makini, na lazima itapanda kushiriki kucheza ligi kuu.

Ameziomba pia Kamati hizo kwamba zifanye kazi yao ipasavyo na mtu ambaye ataonekana kutaka kukwamisha jambo lolote wamsimamishe,huku akitoa ushauri kwa kamati ya usajili kwamba wasisahau kusajili wazawa.

Amesema Mkoa wa Shinyanga ukiwa na Timu ambayo inashiriki kucheza ligi kuu hata uchumi wake utaongezeka,huku akitoa kiasi cha Sh.milioni moja,mipira miwili na set mbili za jezi kwa timu ya Stand United kwa ajili ya kuanza kuwaunga mkono.

2