SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, inatarajia kutoa jumla ya Sh. milioni 280, kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya michezo katika shule 56 zilizopo katika mpango huo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Ofisa Elimu Shule za Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margareth Kapolesya, ambapo alisema kwa upande wa halmashauri yake, ina mpango wa kuboresha miundombinu yao yote ya michezo na si viwanja vya mpira wa wavu (valleyball) pekee.
“Mpango huo ulitokana na uamuzi wetu wa kuiteua Shule ya Sekondari ya Unyahati kuwa ni shule ya mchepuo wa michezo, hivyo ikawa ni miongoni mwa shule 56 za mchepuo wa michezo nchini,” alisema
Kwa mujibu wa ofisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 shule hizo za mchepuo wa michezo nchini, ziliahidiwa kila moja kupewa shilingi milioni tano, lakini mpaka sasa bado hawajapokea kiasi chochote cha fedha hizo.
“Shule hizo za mchepuo wa michezo nchini katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, ziliahidiwa kupatiwa kila shule shilingi milioni tano, lakini mpaka sasa hatujapokea fedha hizo ingawa katika taarifa ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakati wa kufunga michezo ya UMISSETA mwaka 2024 pale mkoani Tabora alisema kuwa tayari shule 28 kati ya 56 zimetumiwa fedha hizo,” alibainisha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED