Vazquez, Nacho na michezo 700, mataji 39 magwiji wasioimbwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:17 AM May 08 2024
Luca Modric, Nacho pamoja na Vazquez.
Picha: Maktaba
Luca Modric, Nacho pamoja na Vazquez.

WAMEUNGANISHWA kwa jumla ya mechi 700 na mataji 39 kwa Real Madrid, lakini Lucas Vazquez na Nacho bado wanaruka chini ya rada, wakiwa na wasifu wa chini sana kuliko wenzao wanaosherehekea.

Katika wiki za hivi karibuni, hata hivyo, wakongwe hao wa muda mrefu wametoka kwenye kivuli na kuchukua majukumu muhimu katika timu yao.

Labda ilikuwa wiki bora zaidi ya kazi ya Vazquez.

Baada ya kutoka kwenye benchi wakati wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Manchester City, akichukua nafasi ya Vinicius Junior wakati wa muda wa ziada, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, alipewa jukumu la kupiga penalti ya tatu ya timu yake na wakatinga nusu fainali.

Vazquez aling'ara zaidi siku nne baadaye Real ilipoikaribisha Barcelona kwenye El Clasico.

Akiwa nafasi ya Dani Carvajal katika nafasi ya beki wa kulia, alishinda penalti kwa bao la kwanza la timu yake, akafunga la pili kwa umaliziaji mzuri mara ya kwanza na kufanya 2-2 na kisha kufanya kazi nzuri kwa kutoa krosi kwa Jude Bellingham aliyefunga bao la ushindi.

Mchezaji huyo wa England alionesha shukrani zake kwa kujiunga na Vazquez kwa mchezo wa kusherehekea na baadaye akachapisha ujumbe mfupi wa mtandao wa kijamii: Lucas Vazquez wewe ni gwiji.

Maelezo hayo si ya kutia chumvi sana, kwa sababu katika muongo mzima uliopita kuwapo kwa Vazquez kwa uthabiti chini ya ubavu wa kulia - ama kama winga wa jadi au beki wa pembeni mbabe - kumekuwa sifa thabiti ya timu inayoendelea kubadilika.

Mzaliwa wa Kaskazini-Magharibi mwa eneo la Hispania la Galicia, Vazquez alihamia mji mkuu na kujiunga na Real akiwa na umri wa miaka 16. Baada ya kufanikiwa kupitia safu ya vijana ya klabu hiyo, alipandishwa ngazi hadi kwenye kikosi cha wakubwa kwa mkopo wa msimu mzima huko Espanyol mnamo 2014-15.

Mara moja alionesha kuwa mchezaji asiyechoka ambaye alichanganya maadili ya timu na matokeo ya kushambulia, alicheza mechi 39 wakati wa kampeni hiyo ya kwanza na alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Real aliporejea.

Tangu wakati huo hajawahi kuwa mbali na hatua hiyo, akicheza angalau mechi 30 kila msimu isipokuwa 2019-20, ambapo alikosa baada ya kuvunjika kidole.

Mbele ya nyota kama vile Gareth Bale, Rodrygo na Carvajal upande wa kulia, Vazquez amekuwa akianza mara Kwa mara. Lakini daima amekuwa tayari kungoja kwa subira zamu yake.

Vazquez anaweza kuwapo kwa muda mrefu zaidi - ingawa mkataba wake unamalizika msimu huu wa majira ya joto, anafikiriwa kuwa karibu kukubaliana na mkataba mpya wa kuongeza muda wake wa kukaa hapo Bernabeu.

Mfungaji mwingine wa penalti aliyefanikiwa katika mkwaju wa penalti dhidi ya City alikuwa Nacho, ambaye alicheza dakika zote 120 kwenye eneo la ulinzi na kufunga mkwaju wa nne kwa kumpeleka maboya Ederson.

Hapo awali alikuwa ametoa uchezaji bora kumzuia Erling Haaland, na jukumu lake kuu katika ushindi dhidi ya mabingwa hao wa England.

Mejeraha ya muda mrefu kwa Eder Militao na David Alaba yamemfanya Nacho kuungana na Antonio Rudiger katika safu ya ulinzi ya kati ya Carlo Ancelotti.

Imani ya Ancelotti kwa Nacho ilisisitizwa mnamo Januari wakati klabu ilikataa kukimbilia soko la uhamisho licha ya majeraha ya Militao na Alaba, badala yake waliweka imani yao kwa Nacho kuongeza kasi.

Na hilo sio jambo jipya, kwa sababu kocha huyo wa Italia amekuwa mtetezi wa hali ya juu wa uwezo mbalimbali wa Nacho, ambaye aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu kutokana na kuondoka kwa Karim Benzema majira ya joto yaliyopita.

Hasa, Ancelotti amempa sifa za kipekee za kuwa beki "asiye kata tamaa" - kila wakati akitarajia mazuri zaidi kutokea, na kwa hivyo kuwa na matarajio muhimu ya kuzima nyakati za hatari ambazo wengine hawangetarajia.

Nacho amekuwa sehemu ya Real Madrid tangu 2001

Mafanikio ya Nacho katika kutengeneza taaluma ya kung'ara ni ya kuvutia zaidi kwa kuwa aligunduliwa kuwa na kisukari akiwa na umri wa miaka 12, mwaka mmoja baada ya kujiunga na kikosi cha vijana cha Real.

Alipuuza ushauri wa awali wa kuacha kucheza soka na sasa anakiri ugonjwa wa kisukari kwa kusaidia kazi yake kukua, na kumlazimu kujifunza katika umri mdogo kuwajibika kwa mwili wake na lishe yake.

Hisia hiyo ya kujitegemea imekuwa ikidhihirika kila mara katika uchezaji wake, huku Nacho akizunguka bila kulalamika pengo lipi la nyuma linalohitaji kujazwa, mara nyingi akisubiri kwenye benchi bila kulalamika.

Onesho lake dhidi ya City huenda lisitoshe kumuweka kwenye timu. Militao sasa yuko fiti tena na anaweza kumtoa Nacho kwa nafasi ya pili.

Kama Vazquez, Nacho mwenye umri wa miaka 34, pia mkataba wake unamalizika msimu huu wa majira ya joto, lakini kuna uwezekano mdogo wa kurejea tena huku kukiwa na uvumi unaomhusisha na kuhamia Italia na Marekani.

Baada ya zaidi ya miaka 20 kwenye vitabu vya Real itakuwa vigumu kusema kwa heri, lakini  kunyanyua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya litakuwa jambo zuri zaidi kwake.