MARA kadhaa watu wanaambiwa waache ulaji vyakula vyenye wanga mwingi, kuepuka maisha bwete ya kukaa bila mazoezi, kufanya mazoezi, kuachana na sukari,mafuta pia kunywa maji mengi ili kupunguza uzito na mafuta mwilini.
Yote hayo sasa , yanaweza kuwa si jambo la kuwahofisha watu. Ni baada ya Dk. Julian Ross, mtafiti mkuu katika Taasisi ya Tiba ya Johns Hopkins ya Marekani kuyabatilisha.
Ross mtaalamu wa afya mbobezi, anasema yote haya ni nusu kweli, hayajathibitika.
“Njia za kupoteza uzito ambazo watu wengi hutumia na zinazoonekana kwenye mitandao kudhibiti uzito, lakini si kwa haraka au kwa kudumu. Kwa sababu hazishughulikii sababu au chanzo cha tatizo.”
Mwishoni mwa wiki Dk. Julian anawataka watu kula wanga kama kawaida. Anasema hivyo kwanini?
Anaeleza kuwa amegundua ujanja wenye mafanikio makubwa na kwamba una nguvu nao ni kutumia binzari ya njano au ‘tumeriki’.
Binzari ni jamii ya mimea kama ilivyo tangawizi isipokuwa ina rangi ya karoti , kama ilivyo tangawizi unaweza kuikausha na kutumia unga wake kwenye chakula.
“Ni rahisi. Nimeigundua ni rahisi kwa kutumia manjano, asilimia 100 ambayo yeyote anaweza kutengeneza nyumbani kwa "kula" au kumaliza mafuta yote tumboni.”
“Maelfu ya watu ambao wamejaribu njia hii ya kujitengenezea nyumbani na manjano wanasema kuwa wamepunguza uzito haraka katika wiki mbili za kwanza, na kugundua kuwa wapengua kwa kasi kwa kula pipi na vyakula wanavyopenda na bila kwenda kwenye mazoezi au lishe ya aina yoyote.”
Wafuasi wa Dk. Julian wameipa mbinu hii jina la utani "Turmeric Hack," kwa sababu ni suluhisho jepesi ambalo hurekebisha tatizo la uzito chapchap kwa kuchoma mafuta ya mwili kikamilifu.
UZITO UNATISHA
Wataalam wanasema ukiwa na uzito kupita kiasi au unene unaopitiliza ni chanzo cha kupata matatizo mengi kiafya kama maradhi ya moyo kwa sababu uzito wa ziada hufanya moyo wako kufanya kazi kwa bidii kusukuma damu, ambayo inaweza kusababisha shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo.
Kiharusi, ikimbukwe shinikizo la juu la damu linaweza kusababisha kiharusi, ambacho hutokea wakati damu inakwama kuingia kwenye ubongo.
Ugonjwa wa kisukari, aidha kunenepa kupita kiasi ni sababu ya hatari kwa ugonjwa wa kisukari cha aina ya pili kinachopatikana ukubwani.
Saratani, inatajwa kwa maelezo kuwa unene huongeza hatari ya kupata aina kadhaa za saratani, ikiwa ni pamoja na saratani ya matiti, koloni na endometriamu au kizazi.
Kukosa usingizi kunaweza kuletwa na uzito wa ziada kwenye shingo unaosababisha ikawa vigumu kupumua usiku na kusababisha kukosa usingizi.
Shinikizo la damu nalo ni zao la uzito wa ziada unaoweza kusababisha mishipa kuwa migumu na kiharusi.
Kadhalika maumivu ya viungo na misuli au maradhi ya ‘ osteoarthritis’, ambayo husababisha maumivu na ugumu katika viungo vya mwili wa mtu mnene.
Ugonjwa wa ini, unaweza kuchochewa na uzito unaosababisha mafuta kujilimbikiza karibu na ini kisha kuharibu tishu ini na kusababisha kovu, na hata ini kushindwa kazi.
Mawe ya nyongo pia yanaweza kutokana na kunenepa kupita kiasi, ambayo hutokea wakati nyongo inapojikusanya na kuwa ngumu kwenye kifuko cha nyongo.
KUITUMIA
Poda ya manjano inaweza kutumika kupunguza uzito kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwenye chai, maziwa na vinywaji vingine binzari ina hiliki, inayosaidia kupunguza uzito kwa kuongeza ‘metaboliki’ au shughuli za mwili zinazotumia chakula kingi lakini ikipunguza hamu ya kula.
Wataalam hao wanashauri kuchemsha maji na kuweka kijiko cha chai cha manjano au binzari inayochemka kwa takriban dakika tano.
Unaweza kuchuja ukitaka, na ili kupata ladha zaidi unaweza kuongeza chai, juisi ya limao au chochote kuanzia mchaichai na ukishauriwa kuinywa wakati hujala chochote ili ifanye kazi kikamilifu.
Aidha, unaweza kuchanganya maziwa na manjano au binzari hiyo, si mbaya kama una asali unashauriwa kunywa kabla ya kulala.
Unaweza pia kuongeza ‘turmeric’ au binzari kwenye chakula kama wali, kachumbari, mboga, supu, kwenye kitoweo au kunyunyiza kwenye karanga na vitafunwa vingine.
Manjano yana kichocheo cha ‘curcumin,’ ambayo inachochea mwili kuchoma kalori kwa ufanisi zaidi. Joto la chai linaweza pia kukata mfumo wa utumbo na kupunguza hamu na tamaa ya kupenda kula zaidi.
Kwa mujibu wataalamu hao ni salama inapotumiwa kwa muda mfupi au mrefu haina athari mwilini. Hata hivyo, inaweza kuchukua miezi kadhaa kuona matokeo makubwa ya kiafya.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED