Watatu toka Chuo cha Ustawi wa Jamii kuwania tuzo ya 'Hult Prize'

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 10:09 PM Jun 08 2024
Wanafunzi wakiwa na mzigo wa taka.
Picha: Mpigapicha Wetu
Wanafunzi wakiwa na mzigo wa taka.

Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam watashiriki shindano la kimataifa la tuzoiitwayo 'Hult Prize', baada ya wazo lao la kibiashara na ubunifu kupenya.

Shindano hilo lilitarajiwa kufanyika jana jijini Nairobi nchini Kenya ambapo wanafunzi hao Hellena Sailas, Maria Daudi na Method Dallu waliwasili jijini humo Juni 5 mwaka huu.

Wazo lao la kibiashara na ubunifu la utengenezaji na uzalishaji wa matofali kwa kutumia taka za plastiki, ndilo limewabeba.

Mkuu wa chuo hicho Dk. Joyce Nyoni amesema, kimekuwa miongoni vyuo vmbalimbali duniani kutoa wanafunzi kuwania tuzo hiyo.

"Tuzo ya Hult ni shindano kubwa zaidi la ujasiriamali wa kijamii kwa wanafunzi duniani, Inayoendeshwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa na timu za wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani," amesema Dk. Joyce.

Amefafanua kuwa shindano hilo linalenga  kutatua tatizo la kijamii lenye umuhimu kwa kuanzisha biashara ya kijamii inayoweza kukua na kudumu.

"Washindi wa mwisho watawasilisha miradi yao mbele ya jopo la majaji mashuhuri, viongozi wa biashara duniani, viongozi wa mawazo na watetezi wa mabadiliko ili kushinda dola milioni  za Marekani na kuanzisha biashara zao," amesema.

Mkuu huyo wa chuo amewapongeza wanafunzi hao kwa wabunifu kwa kuwapa mkono wa kuwatakia mafanikio katika ushiriki wao.