Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo amewataka vijana mkoani Mtwara kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuulinda, kuudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hayo aliyasema jana Aprili 28,2024 wakati akizungumza na Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali katika eneo la Mashujaa park, Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Katika hatua nyingine Jokate, alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Hassan Nyange kuhakikisha vijana waliopewa mikopo ya asilimia 10 kuwatafutia eneo la kufanya biashara.
"Nikuombe mkurugenzi kuwatafutia eneo kikundi hiki cha vijana 'Jitegemee Group' ambacho watafanya kazi zao kwa uhuru bila kubugudhiwa. Kuna viongozi wa upinzani wameanza kutuchokoza vijana tusikubali kuchonganishwa kwa wale wanaotaka kuvùnja muungano,kiongozi atakayefanya asipewe nafasi tuulinde muungano wetu" alisema Jokate
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamis Munkunda akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mtwara amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uwekezaji ikiwemo Bandari ya Mtwara, Hospital ya Kanda, pamoja na kiwanja cha Ndege.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED