Serikali kuangalia uwezekano matumizi akili bandia

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 05:56 PM May 09 2024
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonazi.
Picha: Maulid Mmbaga
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonazi.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na wataalam kutoka Usimamizi wa Sera wa Oxford ‘Oxford Policy Management’ kuhusu uwezekano wa matumizi ya akili bandia katika kufanya mapitio ya matumizi ya umma.

Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dodoma, huku Dk. Yonazi akisema lengo la kikao hicho ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECD) nchini Tanzania.

Awali serikali ilizindua Programu ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) mwaka 2021 kama mpango mkuu wa kuzileta pamoja wizara na wadau mbalimbali ili kuboresha makuzi na maendeleo ya awali ya watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka minane.