Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limezindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia katika Mkoa wa Morogoro kwajili ya kuvitambua vikundi vya kinamama na makundi mengine ili shughuli zao za kijairimali ziweze kunufaika na programa hiyo.
Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng`i Issa alisema hayo wakati wa uzinduzi huo katika Mkoa wa Morogoro kuwa Programa ya Mama Samia inalenga kuwakwamua akinamama kupitia vikundi vyao na makundi mengine ya Watanzania.
`Mkoa huu unafursa kubwa katika kilimo kutokana na ardhi nzuri yenye rutuba na watu wake wengi wanashughulisha na kilimo na shughuli nyingine za kijasiriamali` na shughuli zao zote za kijasirimali wanazofanya tutazitambua alisema.
Issa alifafanua kwamba baraza lake linawaratibu katika mikoa ambapo wanatumika katika kufanyakazi ya kusaidia makundi hayo kuingia katika kanzidata zao ili hatimaye waweze kunufaika na uwezeshaji utakaotolewa na program hiyo.
Aliendelea kusema programa hiyo imekuja kuboresha shughuli zao za kilimo na shughuli zote za kijasiriamali wanazofanya na lengo ni kuwawezesha watanzania kuwa na maisha bora.
Pia aliwataka akinamama katika shughuli zao za kijasirimalia kukumbuka kuweka akiba katika mabenki au katika vibubu ili iwasaidie kupanua biashara zao.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Adam Malima alisema uzinduzi wa programa hiyo ambayo umefanywa na NEEC ni hatua muhimu kwa mkoa wake na hiyo ni moja ya hatua ya serikali katika kufanya watanzania kufanya shughuli za ujasiriamali kwa tija.
`Mkoa wetu umepokea mradi huu wa Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa mikono miwili,‘ na tunaahidi kufanya vizuri zaidim, alisisitiza.Alisema ili kumkwamua mwanamke ni lazima kumpatia uwezeshaji wa mafunzo na uwezeshaji na programa hii imeanza kufanya hiyo na matokeo yake yatakuwa makubwa.
Alifafanua kwamba mkoa wao utatekeleza program ya Imarisha Uchumi ana Mama Samia kwa vitendo, na hiyo itasaidia kuwawezesha watanzania kufanya shughuli za uzalishaji.
Alisema Mkoa wa Morogoro kipaumbele chake kikubwa ni kilimo na wamejipanga kuingiza mbegu za karafuu, michikichi, cocoa na parachichi ambazo watagawa bure mbegu kama njia ya kuyawezesha makundi hayo kuzalisha na kupata utajiri
Alisema shughuli za uzalishaji mazao hayo ya kilimo na shughuli mbalimbali za kijasiriamali zitasaidia watanzania kujikwamua kivipato.
Katibu wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mvomero, Sebastinana Mbaga alisema ujio wa program hiyo ni moja ya hatu ya kuwamua wanawake na makundi mengine kiuchumi.
Alisema katika wilaya yao wanafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi za kijasiriamali za kilimo, kuongeza thamani mazao ya kilimo, uchuuzi na ujasiriamali mbalimbali.
Katika uzinduzi huo baraza likuwa pamoja na taasisi za kifedha ambazo zilitoa elimu namna umuhimu wa kufungua akaunti na kuweka akiba.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED