MGOMBEA Uenyekiti wa Kitongoji cha Stendi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), George Mohamed, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amoni Kakwale, amefika eneo la tukio na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi litahakikisha linawasaka watuhumiwa wote waliohusika na mauaji hayo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Manyoni,Danny Butale, amesema mgombea huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kiunoni baada ya kuvamiwa nyumbani kwake saa 7:00 usiku na kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni baada tukio kutokea.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED