ALIYEKUWA Kada wa Chama cha Mapinduzi, Mchungaji Godfrey Malisa amewataka Watanzania kuacha uoga pale wanapoona haki zao zimevunjwa bali kuchukua hatua ili kutendewa haki.
Katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari nchini, Mchungaji huyo amedai kwamba taifa linaweza kuingia katika matatizo kutokana na ukimya wa wananchi pale viongozi wanapovunja katiba.
“Huwezi kutegemea kufunguliwa mlango kama wewe mwenyewe hujaona umuhimu wa kufunguliwa huo mlango”-amesema Mchungaji Malisa
“Tanzania yetu haitaingia katika matatizo kwa sababu ya wanaopuuza na kuvunja katiba, Chama (CCM) kitaingia kwenye matatizo na Tanzania yetu itaingia kwenye matatizo kama viongozi watavunja katiba na sisi kunyamaza kwa sababu ya uoga” – amesema
Mchungaji Malisa alifukuzwa uanachama katika Chama cha Mapinduzi kwa kile kilichoelezwa ni kupingana na maamuzi ya chama kila wakati.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED