Ajali yaua watu 13 na kujeruhi sita Kilwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:53 PM Apr 22 2024
Ajali ya basi dogo la abiria lagongana uso kwa uso na roli la mafuta Kilwa.
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Ajali ya basi dogo la abiria lagongana uso kwa uso na roli la mafuta Kilwa.

WATU 13 wanadaiwa kufariki dunia na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya Basi dogo la abiria lililogongana uso kwa uso na roli la mafuta katika eneo la Somanga wilayani Kilwa.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Aprili 22, 2024 katika barabara kuu ya Somanga - Nangurukuru 

Majeruhi hao wamepelekwa katika hospitali ya Tingi kwaajili ya matibabu zaidi na pia miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo