WATU wenye silaha kusini-magharibi mwa Pakistan, wamewaua watu saba wakiwa usingizini, katika kile polisi wanakiita kuwa ni tukio la pili la ugaidi wa kikabila katika eneo hilohilo ndani ya mwezi mmoja.
Shambulio hilo limefanyika katika mji tete wa Pwani wa Gwadar ambako mshirika wa kisiasa wa Pakistan China inajenga bandari ya kina kirefu cha bahari, mradi unaopingwa na nchi za Magharibi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi katika eneo hilo, Mohsin Ali amesema walikuwa wakazi wa jimbo la kati la Punjab na kujishghulisha na biashara ya unyozi wa nywele.
Hilo ni tukio la pili kuwalenga watu kutoka Punjab katika eneo hilo la jimbo la Balochistan ambalo linakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo kwa takriban majuma matatu sasa.
DW
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED