Wabunge marekani kupiga kura kumuondoa Spika Mike

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:57 AM May 02 2024
Mbunge wa chama cha Republican Marjorie Taylor Greene aliyemtaka Spika Johnson kujiuzulu.
PICHA: MAKATABA
Mbunge wa chama cha Republican Marjorie Taylor Greene aliyemtaka Spika Johnson kujiuzulu.

WABUNGE wa Marekani watarajia kupiga kura wiki ijayo, ili kubaini kama Spika wa baraza la wawakilishi nchini humo Mike Johnson ataendelea kusalia mamlakani, kwenye mojawapo ya nyadhifa za juu za uongozi katika serikali ya Marekani.

Mike Johnson amekuwa spika tangu mwezi Oktoba mwaka jana na anakabiliwa na tishio kutoka ndani ya chama chake kufuatia Mbunge wa chama cha Republican Marjorie Taylor Greene kumtaka Johnson kujiuzulu siku ya Jumatano, akisema kuwa amesaliti chama kwa kukiuka kanuni zilizofuatwa na Rais wa zamani, Donald Trump na vuguvugu lake la “Ifanye Marekani kuwa Kuu tena”.

Greene amesema ikiwa Johnson hatajiuzulu, ataitisha kura ya kumuondoa.

Juhudi hizo za kiutaratibu, ni za hivi punde zaidi katika nyingine kadhaa zilizibua mtafaruku, za kutaka kumbadilisha spika wa Baraza la Wawakilishi, huku Warepublican wakijaribu kutawala, lakini wakiwa na idadi ndogo ya wajumbe wanaowawezesha kufanya hivyo.

Lakini tofauti na wakati huu wabunge wa wademocrat waliungana na warepublican kumwondoa spika aliyemtangulia Johnso, Kevin McCarthy mamlakani mwaka jana, hali haitakuwa hivyo wakati huu.