Polisi Ufaransa yakamata tani 1.8 ya kokeini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:21 AM May 02 2024
Wakala wa dawa za kulevya akiwa amebeba gunia lenye dawa zilizokamatwa, huku mawakala wakijiandaa kuharibu dawa hizo, nje kidogo ya Jiji la Panama.
Picha: Arnulfo Franco/AP/picture alliance
Wakala wa dawa za kulevya akiwa amebeba gunia lenye dawa zilizokamatwa, huku mawakala wakijiandaa kuharibu dawa hizo, nje kidogo ya Jiji la Panama.

POLISI nchini Ufaransa, imekamata tani 1.8 za madawa ya kulevya aina ya kokeini kutoka katika mashua iliyokuwa imetua nanga kwenye bandari ya Marigot huko kisiwani Saint Martin kilichopo katika utawala wa Ufaransa.

Vyanzo vinaeleza kuwa wahusika katika chombo hicho ambacho kinaelezwa kuwa na injini yenye nguvu kubwa, ambayo inatumiwa sana na wasafirishaji wa magendo walitoroka kabla ya kutiwa nguvuni.

Waendesha mashtaka wa umma katika kisiwa cha hicho cha Ufaransa cha Guadeloupe, wametoa ridhaa ya uchunguzi huo kwa mamlaka ya Saint Martin, kaskazini ambayo inatawaliwa na Ufaransa huku kusini mwa kisiwa hicho ni Uholanzi.

Mwaka 2022, mamlaka ya Ufaransa ilinasa tani 27.7 za kokaine, ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kwa 2021 ingawa muongo uliopita umeshuhudia ongezeko mara tano zaidi, madawa mengi yakiwasilishwa na usafiri wa majini.

DW