Rais William Ruto wa Kenya ametangaza kifo cha Mkuu wa Majeshi nchini humo Gen. Francis Omondi Ogolla ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi 11 wa jeshi la Kenya waliokuwa kwenye ndege ya jeshi la kikosi cha anga aina ya helicopter huku wengine wawili wakinusurika.
Chopa hiyo imeanguka na kulipuka moto katika eneo la Kaber, muda mfupi baada ya kuondoka katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Cheptuel alasiri leo Alhamisi Aprili 18, 2024.
Taarifa kutoka NTV zinaonesha kuwa mamlaka imethibitisha vifo vya watu watano katika ajali hiyo mbaya, huku watatu wakinusurika.
KDF Ogola na viongozi wengine walikuwa katika ziara ya kutathmini hali ya usalama na kujadili uwezekano wa kufunguliwa kwa shule katika eneo la mpaka kati ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet.
Kufuatia kifo hicho Rais William Ruto ametangaza siku tatu za mambolezo kuanzia kesho Aprili 19, 2024.
Chanzo: TUKO.co.ke
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED