Marekani yasitisha kuipelekea Israel msaada wa mabomu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:38 PM May 09 2024
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mazungmzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Picha: Maktaba
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mazungmzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

SERIKALI ya Marekani imesitisha upelekaji wa msaada wa mabomu kwa Israel kutokana na waiwasi kwamba Israel ilikuwa inakaribia kuushambulia mji wa Rafah, kusini mwa Gaza kinyume na matamanio ya Marekani.

Miongoni mwa silaha hizo ni mabomu yenye uzito wa kilogram 900, na kilogram 225.

Shirika la habari la AP limenukuu chanzo cha habari ambacho hakijatajwa kutokana na usiri wa habari hiyo.

Zaidi ya watu milioni 1 wanaishi katika mji wa Rafah baada ya kukimbia Gaza kutokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel Oktoba 7.

Utawala wa Rais wa Marekani, Joe Biden, ulianza kuthathmini msaada wake wa silaha kwa serikali ya Benjamin Netanyahu, baada ya kuonekana kutaka kuivamia Rafah licha ya pingamizi kutoka White house.

VOA