Mafuriko yaua watu 75 na kujeruhi 155 Brazil

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:33 AM May 06 2024
Mafuriko yaliyoikumba Brazil.
Picha: Amanda Perobelli/REUTERS
Mafuriko yaliyoikumba Brazil.

KUFUATIA mafuriko makubwa yaliyolikumba Jimbo la Kusini mwa Brazil la Rio Grande do Sul, yamesababisha vifo vya watu 75 na kujeruhi watu 155, huku wengine 103 wakiwa hawajulikani walipo na wengine zaidi ya 88,000 wakizikimbia nyumba zao.

Hayo yameelezwa na mamlaka za jimbo hilo ambazo zimesema kuwa juhudi za kuwatafuta waliopotea zikiendelea. Mafuriko hayo yametokana na mvua kubwa zilizonyesha mfululizo kwa siku sab ana kusababisha maporomoko ya udongo, kuvunja Barabara na madaraja ya jimbo hilo.

Kati ya hao waliozikimbia nyumba zao, watu wapatao 16,000 wanahifadhiwa kwenye majengo ya shule, kumbi za mazoezi na makazi ya muda. 

Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva amelitembelea jimbo hilo kwa mara ya pili akiwa ameongozana na mawaziri kwaajili ya kukagua uharibifu uliotokea.