BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida limepitisha makadirio ya bajeti ya Sh. bilioni 31.162 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya mishahara,matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo.
Akisoma makadirio ya bajeti hiyo leo Februari 14, 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama,Asia Messos amesema bajeti ya mwaka huu imeongezeka ukilinganisha na ya mwaka 2024/2025, ambapo bajeti ya mwaka huo ilikuwa Sh.bilioni 29.966.
Messos amesema katika bajeti ya 2025/2026 kutakuwa na ongezeko la mapato ya ndani kutoka Sh.bilioni 2.430 mwaka 2024/2025 hadi kufikia Sh.bilioni 3.339 ambalo ni ongezeko la Sh.milioni 908.237 sawa na asilimia 37.36.
Messos amesisitiza kuwa mpango wa bajeti wa mwaka 2025/2026 unategemea kutekeleza shughuli za maendeleo ambazo ni pamoja na miradi ya uwekezaji,kuboresha miundombinu ya mnada wa Kikhonda,kuboresha stendi ya Iguguno na Nduguti na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED