Okash: Vituo vya kupiga kura vipo vya kutosha

By Julieth Mkireri , Nipashe Jumapili
Published at 11:29 AM Sep 15 2024
MKUU wa Wilaya ya Chemba Halima Okash
Picha: Mpigapicha Wetu
MKUU wa Wilaya ya Chemba Halima Okash

MKUU wa Wilaya ya Chemba Halima Okash amewahakikishia wananchi wa Wilaya hiyo kwamba vituo vya kupigia kura vitakuwa vyakutosha vinavyofikika kwa urahisi.

Okash ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na baadhi ya  wananchi wa Kata ya Paranga na Farkwa waliokusanyika kwenye Kijiji cha Kelemaku. 

Akiwa katika Kijiji hicho  Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kujiandaa kutumia haki yao kupiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika mkutano huo wamemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa uhamasishaji sambamba na kusikiliza kero zinazowakabili.

Emmanuel Nakali na Alfa wakazi wa Kelemaku ambao walishiriki katika mkutano huo, wamepongeza hatua aliyochukua Mkuu huyo wa Wilaya kuwafikia wananchi na kusikiliza kero zao huku akiahidi kuzitatua kwa kushirikiana na wataalamu kwenye idara husika.

Okash ameanza kukagua vituo vya kujiandikishia wapiga kura sambamba na kuzungumza na wananchi na anaendelea na ziara hiyo katika Wilaya ya Chemba kata kwa kata lengo likiwa ni kujihakikshia vituo vilivyopo vinafikika kwa urahisi kabla ya kuanza kupiga kura.