MWANAMUZIKI chipukizi wa kizazi kipya, Salim Mkilindi, maarufu kama Rupia Boytz, ameachia singo yake ya kwanza inayoitwa ‘Zigo’ leo na unapatikana katika mtandao wa Boomplay.
Akizungumza na BT, Rupia Boytz, amesema kwamba kazi hiyo ni ya kwanza kuitambulisha kwa mashabiki wa muziki na kwamba imetayarishwa katika ubora unaokubalika.
Amesema wimbo huo ambao umerekodiwa katika studio ya High table ya Barnaba, video yake imeongozwa na Jimmy, utakuwa ni mmoja wa nyimbo bora kutoka kwa wasanii wanaochipukia mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED