Samia asisitiza amani, mshikamano

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 01:22 PM Feb 23 2025
 Samia Suluhu
PICHA:MTANDAO
Samia Suluhu

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesisitiza amani upendo na mshikamano akiwataka Watanzania kumtanguliza Mungu kwa kila jambo.

Ametoa msisitizo huo, alipopita kusalimia katika mashindano ya Quraan yanayofanyika leo jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Taifa.

Akiwa hapo kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tanga katika ziara ya kikazi amewataka watanzania kuwa wamoja na kushikamana akisisitiza ndio nguzo ya nchi.