CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kimemtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu kutogombea ubunge 2025 katika jimbo la Ikungi Mashariki ili kuepuka kupata aibu kama ilivyojitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Joshua Mbana akizungumza leo Desemba 3, 2024 na waandishi wa habari kuhusu ushindi ambao chama hicho kimepata katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, amesema CCM imepata ushindi mkubwa hadi katika kijiji cha Mahambe anachotoka Lissu na kwamba hii inaonesha ni jinsi gani wananchi walivyo na imani na CCM.
"Nimemsikia kaka yangu Tundu Lissu akisema uchaguzi unaokuja 2025 kama hakuna katiba mpya ni bure kwenda kwenye huo uchaguzi,mimi nataka niwaambie katiba haipigi kura kinachopiga kura ni watu,watu hawa wamemuelewa Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka na miradi aliyowapelekea na ndio hao hao watakaopiga kura uchaguzi mkuu 2025," amesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED