DC Magoti: Vijana Jeshi la Akiba msijiingize kwenye makundi ya kisiasa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:23 PM Nov 02 2024
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti akiwa na Askari wa Akiba.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti akiwa na Askari wa Akiba.

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti ametoa wito kwa Vijana wa Jeshi la Akiba kutojiingiza kwenye makundi ya siasa mara baada ya kuhitimu Mafunzo yao bali kufata vifungu vya sheria za Jeshi hilo la Akiba.

Mkuu wa Wilaya huyo ameyasema hayo wakati wa kufunga mahafali ya Miezi Minne kwa Askari wa Jeshi la  Akiba (Mgambo),mkoani Pwani amesema 
Askari hao wanapaswa kujiadhari kwa kiasi kikubwa  na maneno ya wanasiasa kwani ni rahisi kuwapotosha

"Ninaomba niwaase ,Jeshi la Akiba  mtambue mpo chini ya vifungu vya Sheria hivyo  msikubali kutumika kisiasa kwa namna yoyote ile hakikisheni mnalinda 
heshima za Jeshi,viapo vyenu,nidhamu mliyofundishwa  na Uzalendo wa taifa letu,"amesema.

Amesema askari hao wanapaswa kusimamia Taifa ,Mikoa na Wilaya ipasavyo na kuwa macho kwa serikali katika kutoa taarifa za kihalifu hususan za  ubadilifu wa maliasiri za nchi na nyara za serikali.

"Popote mtapoona zinatumika vibaya katika maeneo mtakayoishi, mtatoa taarifa juu ya mtu yoyote ambaye anahatarisha hali ya usalama katika maeneo yenu katika uchochezi wa masuala ya kisiasi na ugaidi,"amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti.
Kwa Upande wake Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Kisarawe, Meja Silvery Mabubu  amesema miongoni mwa changamoto zinazowakumba katika mafunzo hayo ni pamoja na  ufinyu wa bajeti uliopo.

"Tunamshukuru sana Mh.DC kwa  uongozi wake kutusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo suala la usafiri na mafuta pindi ya kozi hii ikiwa inaendelea,"amesema.

Amesema wanapendekeza halmashari ianze kuwazingatia katika  bajeti hata wakikusanyiwa kiasi cha fedha  kidogo kidogo hadi hapo wanapoanza kozi nyingine itakuwa inawasaidia katika  kupata zana za kufundishia na maandalizi ya porini.

Kozi hiyo imefanyika kwa muda wa wiki 16 katika Kata ya Manerumango iliyopo wilayani Kisarawe Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Petro Magoti akiwa na Askari wa Akiba.