JESHI la Polisi nchini limesema linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za wizi wa Madaftari mawili ya Wakazi katika Kituo cha Josho, Kijiji cha Kikelelwa kata ya Tarakea Motambu wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
“Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu njama zilizopangwa na chama kimoja cha siasa za kuvamia na kupora vitabu vya kuandikisha wapigakura kwa madhumuni wanayoyajua wao wenyewe. Tunatoa tahadhari kwa waliokaa na kupanga uhalifu huo kuwa ni kosa kisheria lakini wasithibutu kutekeleza njama hizo kwani hatua kali kwa mujibu wa sheria zilizochukuliwa dhidi yao,”amesema Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Davidi Misime katika taarifa yake kwa umma.
“Jeshi la Polisi lingependa kuwahakikishia wananchi kuwa limejipanga vizuri kuhakiksiha uandikishaji unakamilishwa vizuri leo na ambao wajajajiandikisha wasisite kujitokeza kujiandikisha bila hofu yeyote.”
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema TAMISEMI imekubali kuongeza muda kwa wananchi wa eneo hilo kujiandikisha upya, na kwamba utaanza leo Oktoba 20,2024 hadi Oktoba 28, mwaka huu.
Unandikishaji wa wapiga kura ulianza Oktoba 11 na umekamilika jana, huku wagombea wataanza kuchukua na kurejesha fomu Novemba mosi hadi 7, 2024.
Aidha, mikutano ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa utanaanza Novemba 20 hadi 26, mwaka huu, huku uchaguzi ukifanyika Novemba 27, 2024.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED