RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Baba wa Taifa la Namibia na Rais wa Kwanza wa taifa hilo, Sam Nujoma.
Ametuma salamu za rambirambi kwa Wanamibia kutokana na kifo hicho.
Nujoma (95), amefariki dunia jana, jijini Windhoek nchini humo, akiwa ni miongoni mwa wapigania uhuru na wanaharakati wa ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, walioungwa mkono na Mwalimu Julius Nyerere.
“Mpigania uhuru, Mwana-Pan-Africanist, na rafiki wa dhati wa Tanzania ambako aliwahi kuishi wakati wa harakati za uhuru wa Namibia.
Rais wa Namibia, Dk. Nangolo Mbumba, amesema nchi hiyo itatangaza maombolezo ya kitaifa.
Amesema Nujoma alifariki kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili baada ya kulazwa hospitalini kwa wiki tatu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED