MTANGAZAJI mkongwe wa Radio na Television hapa nchini, Bujaga Izengo Kadago, ameufagilia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutokana na kutoa huduma kwa ufanisi.
Kadago ambaye ni mstaafu anayepokea pensheni kutoka PSSSF, ameyasema hayo wakati wa Kikao Kazi baina ya PSSSF na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro (Morogoro Press Club), mjini Morogoro Desemba 14, 2024.
Amesema alipostaafu utumishi wa umma mwaka 2019 alipata ushirikiano wa kutosha wakati wa mchakato wa kupatiwa malipo yake.
“Nililipwa kwa wakati, kwakweli ninachoweza kusema huduma zenu ni safi na za kuridhisha.” amesisitiza Bujaga ambaye kwa sasa anatangaza kwa mkataba TBC Taifa.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF,Yesaya Mwakifulefule, amesema kikao hicho ni utaratibu wa Mfuko kukutana na wadau wakiwemo waandishi wa habari, ili kuwaelimisha kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko.
“Tunahitaji kuendeleza uhusiano na morogoro press club na klabu za waandishi wa habari nchini kwa lengo la kuwafikishia taarifa wanachama wa PSSSF vizuri.” amesema
Aidha, amewahakikishia waandishi hao w ahabari kuwa Mfuko uko vizuri, na unalipa mafao kwa wakati.
“Uwekezaji wa mfuko unaendela vizuri na sehemu kubwa ya nyumba za kupangisha kwa sasa zinawapangaji.” amesisitiza Mwakifulefule.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED